Picha: Kuapishwa kwa George Weah kulivyofana

Mwanasoka wa zamani wa Liberia, George Weah ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

Weah amechukua nafasi ya Rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf ambaye amestaafu.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na wanasoka, Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo.

Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d’Or.

Related Articles

Back to top button