Michezo

Picha: Manchester United yaivuta shati Chelsea katika mbio za ubingwa wa EPL

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford dakika ya saba alianza kuifungia timu yake goli moja katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.

Rashford akishangilia goli lake akiwa na wachezaji wenzake

Ander Herrera dakika ya 49 aliipatia Manchester United bao la pili na kuufanya mchezo huyo kumalizika kwa Man U kushinda 2-0.

Pamoja na kufungwa, Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 75 za mechi 32 wakati United inaendelea kushika nafasi ya tano kwa pointi 60 za mechi 31

Katika Mechi nyingine tunamshuhudia Roberto Firmino akiipatia Liverpool bao dhidi ya West Brom na hivyo Liverpool wanachupa sasa katika nafasi ya tatu ya Premier League.

Valencia (kushoto) akimtoka kiungo mkabaji wa Chelsea, Ngolo Kante

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents