Picha: Mrembo wa Ufaransa atwaa taji la Miss Universe

Mrembo mwenye miaka 23, kutoka Ufaransa, usiku wa kuamkia Jumatatu, ametwaa taji la Miss Universe, shindano lililofanyika nchini Ufilipino.

Iris Mittenaere kutoka jiji la Lille, aliibuka mshindi kwenye shindano hilo lililokuwa na washiriki 86.

Mittenaere amerithi taji hilo toka kwa mshindi wa mwaka jana, raia wa Ufilipino, Pia Wurtzbach.

Nafasi ya pili imekamatwa na Miss Haiti, Raquel Pelissier na ya tatu kwenda kwa Miss Colombia, Andrea Tovar. Tanzania iliwakilishwa na Jihan Dimack.

Related Articles

Back to top button