Michezo

Picha: Tuzo za Kili Music 2013 zazinduliwa rasmi

Baraza la sanaa la Taifa, BASATA na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo wamezindua rasmi tuzo za muziki za Tanzania zijulikanazo zaidi kama Kili Music Awards kwa mwaka 2013.

Mkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas (katikati) na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakidhamini mkataba mpya wa miaka mitano wa udhamini wa bia ya Kilimanjaro katika tuzo hizo
Mkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas (katikati) na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakisaini mkataba mpya wa miaka mitano wa udhamini wa bia ya Kilimanjaro katika tuzo hizo

Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam bia ya Kilimanjaro ambayo ndio wadhamini wakuu wa tuzo hizo wamesaini mkataba mpya wa miaka mitano na BASATA wa kuzidhamini ambapo zaidi ya shilingi bilioni 4 zitatumika kuziandaa kwa kipindi hicho.
IMG_7401

IMG_7407

IMG_7413

Tuzo za mwaka huu zitafanyika tarehe 8 June kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

“Lengo hasa la kusaani mkataba huu ni kuwahakikisha watanzania kuwa tutaendelea kuwapa tuzo hizi na tutaendelea kuzifanya kwa kusikiliza matakwa ya wadau wa sanaa ya muziki Tanzania wanataka nini ili sisi kama wadhamini kuhakikisha wanakipata kile wanachokitaka,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza kwenye uzinduzi huo
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza kwenye uzinduzi huo

IMG_7389

Kavishe amesema tuzo za Kilimanjaro ni miongoni mwa tuzo kubwa kabisa za muziki barani Afrika.

“Wale wanaofuatilia tuzo za muziki Tanzania, barani Afrika na duniani kwa ujumla mtakubaliana na mimi kabisa kwamba tuzo hizi kwa hapa Tanzania na kwa Afrika kwa ujumla ni za ukubwa kuliko tuzo zote zinazotolewa, ilikuwa inatanguliwa na Kora Music, MTV na Channel O awards.”

Nembo rasmi ya tuzo za Kili mwaka 2013
Nembo rasmi ya tuzo za Kili mwaka 2013
Maafisa wa TBL na BASATA wakizindua nembo ya tuzo za mwaka huu
Maafisa wa TBL na BASATA wakizindua nembo ya tuzo za mwaka huu
Mkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakizindua nembo ya Kili Music Awards
Mkurugenzi wa masoko wa TBL kushilla Thomas na Kaimu Mkuu Mtendaji wa BASATA Godfrey L. Mngereza wakizindua nembo ya Kili Music Awards

IMG_7419

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey L. Mngereza alisema juhudi za BASATA na wadhamini wa tuzo hizo, zimeifanya serikali iitambue rasmi tasnia ya muziki kama shughuli rasmi. “Kwahiyo tasnia ya muziki ni rasmi kuanzia January mwaka huu,” alisema Mngereza.

“Baraza linachukua fursa hii kuwaasa wasanii kuthamini program hii na kuongeza ubunifu wa kazi zao ili ziwe katika viwango vya kitaifa na kimataifa.”

IMG_7431

IMG_7438

IMG_7439

IMG_7441

IMG_7444

IMG_7449

Katika uzinduzi huo nembo rasmi ya tuzo za Kili mwaka 2013 ilizinduliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents