HabariPicha

Picha: Vijana wawili walioweka rekodi ya kumchora Obama

Vijaana wawili nchini Marekani ambao ni wasanii upande wa uchoraji wamekka rekodi kwa kuchora picha ya Rais Mstaafu wa nchi hiyo Barack Obama pamoja na mkewe Michell Obama.

Wasanii hao Kehinde na Sherald wamekuwa wasanii wa kwanza Weusi kuchora picha ya Rais ambayo itatumika katika makumbusho. Obama kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika machache kuhusu hilo;

Leo, @KehindeWiley na @ASherald wamekuwa wasanii wa kwanza weusi kuunda picha rasmi ya Rais katika makumbusho ya Smithsonian .

Shukrani kwa Kehinde na Amy na vizazi vya Wamarekani pamoja na vijana wote kutoka duniani kote wataotembelea hifadhi hii ya Taifa na kuona picha ya nchi.

Wakishatembelea makumbusho hayo wataondoka wakipata maana nzuri zaidi ya kuipenda Marekani. Na ninamatumaini kuwa wakishatembelea watatoka na uwezo zaidi wa kwenda kubadili ulimwengu wao.

Kehinde amechora picha ya Obama wakati Sherald akichora picha ya Michelle.

Kehinde akiwa na Obama

Picha ya Obama iliyochorwa na Kehinde

Michelle Obama akiwa na Sherald

Picha ya Michelle iliyochorwa na Sherald

Related Articles

Back to top button