Michezo

Pilato wa mechi ya FA: Yanga vs Simba

Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara ndiye aliyepangwa kusimama katikati katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup kati ya watani wa jadi, Yanga vs Simba utakaochezwa Mei 28, 2022 kwenye Dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

Waamuzi wasadizi katika mchezo huo watakuwa ni Frank Komba na Mohamed Mkono huku Elly Sasii akiwa ni mwamuzi wa akiba (fourth Official).

Kwa upande wa nusu fainali ya pili itakayowakutanisha Azam FC vs Coastal Union, mwamuzi wa kati atakuwa Ramadhan Kayoko, akisaidiwa na Frednand Chacha na Soud Lila wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kassim Mpanga.

Related Articles

Back to top button