Michezo
Pilato wa Simba huyu hapa dhidi ya Jwaneng
Siku ya Jumamosi, machi 02, Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam kucheza na Jwaneng Galaxy ikihitaji ushindi ambao utaifanya ijihakikishie nafasi ya pili kwenye kundi B na kutinga robo fainali, ikiwa na pointi nane.
Mchezo kati ya Simba na Jwaneng Galaxy itakuwa chini ya usimamizi wa refa Daniel Nii Laryea kutokea Ghana, refa huyu amewahi kuchezesha mechi moja ya Simba ambayo ilikuwa ugenini ni dhidi ya RS Berkane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mnamo February 27, 2022 ambayo Wekundu wa Msimbazi walipoteza kwa Mabao 2-0.
Imeandikwa na Mbanga B.