Pogba afanya mazungumzo na Rais wa PSG

Kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, amefanya mazungumzo na rais wa Paris St-Germain, Nasser Al-Khelaifi lakini klabu hiyo ya Ufaransa inasisitiza kuwa haikuwa kitu zaidi ya kukutana tu.

Taarifa zinadokeza kuwa Pogba, anatarajiwa kutimka Old Trafford na kujiunga na matajiri hao wa Ufaransa PSG msimu ujao baada ya kushindwa kuingia makubaliano mapya.

Pogba atakuwa mchezaji huru ifikapo mwishoni mwa msimu huku idadi ya timu zinazoonyesha nia ya kumuhitaji zikizidi kuongezeka ikiwemo miamba ya soka Hispania klabu ya Real Madrid.

Related Articles

Back to top button