Habari

Poland yashinikiza Ujerumani kulipa fidia uharibifu wa vita vya pili vya dunia

Serikali ya Poland inataka kuongeza shinikizo dhidi ya Ujerumani kuhusu suala la kulipwa fidia ya vita vya pili vya dunia.

Kwa mujibu wa naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Arkadiusz Mularczk, Poland inataka kufikia lengo lake hilo kwa sababu ni muhimu kwa nchi hiyo na sio suala la kisiasa.

Naibu waziri huyo wa mambo ya nje wa Poland pia amesisitiza kwamba Ujerumani inaweza kuchagua ama kukaa kwenye meza ya mazungumzo au Poland italiibua suala hilo katika majukwaa yote ya kimataifa katika Umoja wa Mataifa, baraza la Ulaya na katika Umoja wa Ulaya.

Mularczyk ambaye pia ni mwenyekiti wa tume maalum ya bunge nchini Poland kuhusu suala hilo amesema kuna ripoti iliyoandaliwa kuhusu uharibifu uliofanywa dhidi ya Poland na utawala wa Wanazi wa wajerumani wakati wa vita vya pili vya dunia. Uharibifu huo unafikia dola Trilioni 1.3.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents