Habari

Polisi kuwaska waliosambaza taarifa za Uongo

Jeshi la Polisi linapenda kuwajulisha umma kuwa kuna taarifa za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili zilizokuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jeshi la Polisi (tanpol) kwa lengo la kutaka kuuaminisha umma kuwa zimetolewa na Jeshi la Polisi kupitia mtandao wake wa X.

Taarifa hizo si za kweli na ifahamike kuwa Jeshi la Polisi haliwezi kuandaa na kusambaza taarifa kama hizo katika Mitandao yake ya kijamii.

Wakati tunaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe, tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza endapo zitakufikia.

Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote yule aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa tarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza.

Credit by @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents