Polisi lawamani kwa kukamata wasio wahalifu

WIKI moja kabla ya kuja nchini kwa Rais wa Marekani, George W Bush, Jeshi la Polisi limeanza kufanya msako wa kuwakamata watu mbalimbali bila sababu za msingi, kitendo kilicholalamikiwa na wakazi wengi wa Dar es Salaam.

na Prisca Nsemwa

 

WIKI moja kabla ya kuja nchini kwa Rais wa Marekani, George W Bush, Jeshi la Polisi limeanza kufanya msako wa kuwakamata watu mbalimbali bila sababu za msingi, kitendo kilicholalamikiwa na wakazi wengi wa Dar es Salaam. Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, walisema kuwa kuja kwake kusisababishe watu wasio na hatia kukamatwa kwa kuhusishwa na vitendo wasivyovifanya.

 

Steven Charles, mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, alisema kuja kwa kiongozi huyo wa Marekani kusisababishe Watanzania kukaa kwa hofu katika nchi yao.

 

Aliongeza kuwa kitendo hicho cha polisi kukamata watu hovyo, kinaathiri baadhi ya shughuli za maendeleo kutokana na ndugu za wananchi hao kutumia muda mwingi kushughulikia matatizo yaliyowapata nduo zao.

 

“Kwa nini tusumbuliwe katika nchi yetu wenyewe, kuja kwake kusituathiri sisi wazawa, kama anakuja aje kwa kazi zake kisha aondoke, lakini hakuna sababu ya watu kukamatwa kwa kudhaniwa kuwa ni wahalifu, hilo siliafiki,” alisema Charles.

 

Ashura Shabani wa Buguruni alisema kitendo hicho ni cha kikatili na cha kudhalilisha Watanzania.

 

Alitoa wito kwa jeshi hilo kuacha tabia ya kuwakamatakamata watu ovyo hasa watu wasio na hatia, kwa madai kuwa wanasafisha jiji kiasi ambacho kinawasababishia wananchi usumbufu.

 

Mwanzoni mwa wiki hii, jeshi hilo kupitia kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, waliahidi kuimarisha usalama katika kipindi chote cha ziara ya Rais Bush.

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents