Klabu ya Polisi Tanzania imefikia makubaliano na aliyekuwa kocha wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo.
Makubaliano baina ya Kocha Mwinyi Zahera na Uongozi wa Klabu hiyo umefikiwa hii leo mkoani Kilimanjaro baada ya mazungumzo muda mrefu ya pande zote mbili.