Siasa

Polisi wafyatua mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji Kenya

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya wamewarushia mabomu ya kutoa machozi wakaazi wa kitongoji duni kikubwa zaidi katika mji mkuu wa Nairobi, ili kuwazuia kuandamana hadi katikati mwa jiji kwa ajili ya maandamano yaliyopangwa na upinzani.

Imeelezwa kuwa kuna msururu mkubwa wa polisi mjini humo na njia za kuelekea kwenye makazi rasmi ya rais zimezuiwa.

Baadhi ya wazazi wamechagua kuwazuia watoto wao wasiende shuleni siku ambayo masomo yalikusudiwa kuanza tena baada ya mapumziko ya katikati ya muhula.

.

Milolongo mifupi imeshuhudiwa katika mitaa ya Nairobi kabla ya maandamano yaliyopangwa.

Barabara zinazoelekea Ikulu zimefungwa huku polisi wakielekeza baadhi ya magari kurejea yalikotoka na kutafuta njia mbadala.

.
.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents