Habari
Polisi wamsaka alieweka Dawa ya Nguvu za Kiume kwenye Maji ya Kanisani
Polisi Mjini Bulawayo nchini Zimbabwe, wameanzisha msako mkali wa kumtafuta kijana aliyeweka dawa ya kuongeza nguvu za kiume maarufu kwa jina la (Viagra) kwenye Tanki la maji la kanisa wakati wa Ibada.
Mshukiwa ametambuliwa kwa Jina la Tracy Sibanda mwenye umri wa miaka 18 na inasemekana alitekeleza unyama huo siku ya Pasaka na kuzua Taharuki ndani ya kanisa hilo.
Haijaeleweka bado kijana huyo alitoka wapi na wazo hilo la kifedhuli.
Imeandikwa na Mbanga B.