BurudaniHabari

Post Malone baada ya kudondoka jukwaani aeleza kuendelea vizuri

Post Malone ametuma ujumbe kwa mashabiki wake, kuwafahamisha kuwa yuko sawa … huku pia akielezea ni nini hasa kilifanyika kusabbaisha adondoke jukwaani.

Mwimbaji huyo anasema wakati wa show yake hiyo ya acoustic  kuna eneo kwenye jukwaa ambalo huachwa wazi kwa lengo la kupitisha  vyombo vya chini endapo kuna set inatakiwa iwekwe wakati show inaendelea.

Jambo ambalo inaonekana alisahau alipokuwa akizunguka na kuanguka ndani yake.

Post alishukuru umati wa watu kwa kupaza sauti kupinga taarifa za uongo na kueleza kuwa kwenye jukwaa hilo kulikuwa na shimo kubwa kwenye na pia kuomba radhi kwa kukatisha show yake.

Related Articles

Back to top button