Prince Harry afunguka jinsi kifo cha mama yake Princess Diana kilivyomtesa kwa miaka 20
Prince Harry wa Uingereza, ameeleza kuwa alitafuta ushauri nasaha miaka minne iliyopita kukabiliana na huzuni ya kumpoteza mama yake, Princess Diana.
Kwenye mahojiano na gazeti la Uingereza la The Telegraph, Harry amesema kumpoteza mama yake katika umri mdogo kulisababisha aishi maisha ya hovyo. “Naweza kusema kuwa kumpoteza mama yangu nikiwa na miaka 12 na hivyo kuzima hisia zangu zote kwa takriban miaka 20, kumekuwa na madhara makubwa, si tu katika maisha yangu binafsi bali pia kazi yangu,” alisema kwenye mahojiano hayo yaliyochapishwa Jumapili.
Prince Harry amesema alitafuta ushauri wa kitaalamu akiwa na miaka 28 baada ya kupitia miaka miwili ya vurugu. “Sikujua nilikuwa na tatizo gani. Njia yangu ya kukabiliana nalo ilikuwa ni kukiweka kichwa changu kwenye mchanga. Kukataa kamwe kumfikiria mama yangu kwasababu kwanini hiyo isaidie? Itakufanya tu uwe na huzuni. Haiwezi kumrudisha tena,” alisema.
Princess Diana alifariki kwa ajali ya gari mjini Paris August 31, 1997. Kifo chake kilisababisha mshtuko mkubwa na kuiweka Uingereza katika kipindi kirefu cha maombolezo.
Akijulikana na kama princess wa watu, Diana alifunga ndoa na Prince Charles kwenye harusi ya kifahari katika kanisa la St. Paul mjini London mwaka 1981. Alimzaa mwanae wa kwanza William mwaka 1982, na wa pili, Harry, 1984.
Harry alipata shida kukabiliana na macho ya vyombo vya habari. Miaka mitano baada ya kifo cha mama yake, akiwa na miaka 16, baba yake alimpeleka rehab, siku moja baada ya kukiri kunywa sana pombe na kuvuta bangi.
Baada ya alijiunga na jeshi la Uingereza na kumaliza July 2015.