Burudani
Producer Abbah amtambulisha msanii mpya Bytar, afananishwa na Burna Boy (Video)
Mtayarishaji wa muziki @abbah_process ambaye amemtengeneza msanii kama @marioo_tz na wengine, wiki hii amemtambulisha msanii wake mpya @bytar_beast ambaye yupo chini ya Abbah Music ambayo inafanya kazi na wasanii wengi. Msanii huyo mpya ambaye ametambulishwa na wimbo mpya uitwao Gimme Love, amesema amejipanga kufanya vitu vikubwa kwenye muziki kwa kufanya vitu tofauti.