Burudani

Producer Manecky ashutumiwa kuuza beat mara mbili



Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro 2012 katika kipengele cha producer bora Manecky wa AM Records, anashutumiwa kwa kuiuza beat iliyokuwa imenunuliwa na msanii mchanga wa hip hop aitwaye Brian kwa Izzo B.
Beat hiyo ni ile iliyotumika kwenye wimbo wa Izzo Bizness uitwao ‘Mwaka Jana’.
Katika mahojiano ya kushtukiza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm kati ya Brian na Izzo B yaliyokuwa kama drama, Izzo B alichukizwa na kile alichokiita ‘kutumiwa na msanii huyo ili ajipatie umaarufu’.
Katika utetezi wake, Izzo ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Simwinga alisema beat hiyo alipewa siku ya kikao cha kwanza cha tuzo za Kili kilichofanyika Benjamin Mkapa Towers.
Alisema wakati wakila chakula cha mchana, Manecky alimwambia Izzo kuwa anayo beat kali na hivyo kumtumia kwenye simu kwa njia ya BBM.
Alidai kuwa wakati wanaondoka, aliisikiliza beat hiyo kwa kutumia headphones za Jay Moe. Aliipenda na hivyo kurekodi wimbo wake ‘Mwaka Jana’ kwa kutumia beat hiyo siku nne baadaye.
Kwa upande wake Brian alidai kuwa baada ya kumlipa shilingi laki tatu Manecky aka Necky Boy, aliingiza sauti za mashairi yake lakini shughuli ikaja kwenye kufanyiwa mixing.
Brian alisema alijaribu kumpigia simu producer huyo lakini mara nyingi alikuwa hapokei simu yake na hiyo ni baada ya kumwambia kuwa tayari beat hiyo imetumiwa na Izzo ambaye alikwenda kufanya sauti kwenye studio nyingine.
Baada ya kuusikia wimbo wa Izzo B ukichezwa ndipo naye alipoamua kwenda kuufanya sehemu nyingine kwa kutumia beat hiyo.

Hata hivyo Izzo B akiongea kwa jaziba, alisema hawezi kumkataza Brian kuitumia beat hiyo na hapendi kuendelea kutajwa redioni na msanii huyo kwakuwa mwenye kosa si yeye bali ni Manecky.
“We rekodi fanya video mimi nakupa blessing”, alisema Izzo.
Hata hivyo imebainika kuwa hiyo sio mara ya kwanza kwa Manecky kugawa beat mara mbili kwani kuna msanii wa kike wa Zanzibar aliwahi kulalamika kuwa beat ya Mawazo ya Diamond ilikuwa yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents