Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMuziki

Producer Mocco aingia rasmi kwenye muziki, aachia wimbo mpya

Takriban miaka sita 6 toka niingie kwenye kiwanda cha muziki upande wa audio production..

nikiwa kama producer imekuwa safari nzuri sana kwenye maishayangu namshukuru Sana Mungu kwa kila hatua pia nawashukuru sana wote mnaopokea kazi zangu nakuzisapot ..

Lakini pia nilikuwa natamani siku moja watu wasikie upande wa pili wa talanta yangu nyingine hapa nazungumzia Upande Wa Uimbaji kwani ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu Sana .. hivyo basi ninafuraha kubwa sana kuwakaribisha mashabiki na wadau wa muziki siku ya kesho ijumaa ya tarehe 24/6/2022 kwa mara ya kwanza nitawaletea wimbo wangu wa kwanza ambao utapatikana kwenye digital platforms zote Duniani..

Ombilangu kwenu nilikua naomba mnipokee kijanawenu kama jinsi mlivyo nipokea kwenye production napenda kutanguliza neno la asante kwenu na Mungu awabariki sana

#Moccogenius #imaginationSound

Related Articles

Back to top button