Producer wa Aiyola ya Harmonize kutayarisha wimbo wa Olamide wa Nigeria

Producer wa wimbo ‘Aiyola’ wa msanii wa WCB, Harmonize, Maximizer amelikuna sikio la msanii wa Nigeria, Olamide.

61e3fcba-ec6a-4aa3-8590-d4b933dd15a3
Producer Maximizer

Meneja wa studio ya Kazi Kwanza ambayo Maximizer anafanyia kazi, Lawize ameiambia Bongo5 kuwa Olamide aliupenda wimbo Aiyola baada ya kuona wasanii wengi wakubwa Nigeria wakiupost Instagram na akapenda afanye naye kazi.

Amesema wawili hao waliwasiliana kwenye email na Olamide anatarajia kufanya ziara Afrika Mashariki mwezi ujao atakapotumia nafasi hiyo kufanya kazi na Maximizer.

Olamide
Olamide

Kabla ya kufanya kazi kwenye studio za Kazi Kwanza producer huyo alikuwa akifanya kazi kwenye studio za Mazu Records ambako alitayarisha nyimbo kibao zikiwemo Pacha Wangu ya Rich Mavoko, Nakumiss ya Timbulo, Msondo Ngoma ya Nuh Mziwanda na zingine.

Akiwa Kazi Kwanza, pamoja na kazi zingine, producer huyo ametayarisha nyimbo zote za rapper wa kike, Chemical.

Related Articles

Back to top button