Burudani
Producer wa Harmonize ‘Producer Bonga’ aondoka Konde Gang, asaini kwenye label mpya

Mtayarishaji wa Muziki, Producer Bonga ambaye alikuwa anafanya kazi kwa ukaribu na muimbaji Harmonize ameamua kuanza maisha mapya kama msanii wa muziki chini ya label ya Lykos Empire. Msanii huyo ametangaza uamuzi huo mbele ya nyombo vya habari huku akidai amechota mengi mazuri kutoka kwa bosi huyo wa label ya Konde Gang.