Habari

Promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers yawazaidia wanafunzi na shule zao

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi za jijini Dar es Salaam pamoja na shule zao wamejishindia zawadi mbalimbali ambazo ni pamoja na kompyuta, kompyuta mpakato (laptop) na Baiskeli za kisasa baada ya kushiriki katika promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers, promosheni ambayo iligusa maisha ya zaidi ya wanafunzi 500,000 na shule zao.

Promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers ilikuwa ikiendeshwa na kampuni ya AVI International, ambayo ilikuwa inalenga kuendelea kuhamashisha na kujenga ufahamu wa bidhaa za Bakers ambazi ni biscuit huku ikiendelea kujikita kwenye soko.

Vigezo vya kuwapata washindi vilikuwa ni kuwapa motisha wazazi na walezi kununua biskuti za bakers kwa ajili ya watoto wao nyumbani na kwa shuleni pia, jambo ambalo pia liliwawezesha walimu, na shule kujishindia zawadi ambazo ni pamoja na kompyuta, kompyuta mpakato (laptop), Baiskeli za kisasa pamoja na mabeg ya shule. Shule na wanafunzi waliokuwa na idadi kubwa ya tokeni walitangazwa kuwa washindi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi, Mwakilishi wa Bakers Ltd Frikkie Van Niekerk alisema shindano hilo liliwapa wanafunzi fursa nzuri ya kujifunza kuhusu virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye biskuti za Bakers kwa ukuaji wao, na kuwasaidia kufikia ndoto zao za kuwa na maisha bora ya baadaye.

“Tumefurahishwa na idadi kubwa ya shule na wanafunzi walioshiriki katika promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers.”Napenda kuwashukuru wote walioshiriki na ninawapongeza wale ambao tunaowakabidhi zawadi.

Kwa wale ambao hawakuweza kujishinda kwa siku ya leo naomba niwafahamishe kuwa sisi zote tumekuwa ni washindi. Kushiriki kwenye promosheni yetu tayari tumekuwa washindi na naomba nichukie fursa hii niwajulishe ya kwamba sisi Bakers tutaendelea kuja na promosheni zaidi kwa ajili ya wanafunzi wetu.

Alitaja Shule za Msingi ambazo zilizoibuka washindi kuwa ni Shule ya Msingi Mbezi Beach iliyojinyakulia kompyuta tatu na kompyuta mpakato moja (Laptop), Shule ya Msingi Misewe iliyojishindia kompyuta mbili na kompyuta mpakato moja (Laptop) huku Shule ya Msingi Kigamboni ikiwa ya tatu na kushindia kompyuta moja na Laptop moja.

Wanafunzi watano bora walioshinda Baiskeli za kisasa ni Hassan Musin kutoka shule ya Msingi Mbezi Beach, Marcus Jacob Urasa kutoka shule ya msingi ya Mgulani, James Joseph na Gloria Dickson kutoka shule ya msingi Jaica na Bakary Salum kutoka shule ya msingi ya Amani. Wanafunzi wengine 25 waliweza kujishindia mabegi ya shule.

‘Naomba nitumie fursa hii kuhimiza shule ambazo zimeshinda kompyuta na kompyuta mpakato kuzitumia ipasavyo katika kukuza ujifunzaji wa kidijitali katika shule zao. Sote tunaelewa jinsi ujifunzaji wa kidijitali umekuwa muhimu sana katika shule zetu kwani huwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa kidijitali katika umri wao mdogo. Aidha itasaidia walimu katika kurahisisha kuzalisha nyenzo za kufundishia na kutoa mbinu mpya za kufundishia, alisema.

Akizungumza kwa niaba ya shule zilizoshinda, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi Beach xxxx aliipongeza kampuni ya Bakers Ltd kwa kuja na promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers akisema kuwa imesaidia kuboresha mazingira yao ya kufundishia kwani pamoja na Kompyuta na Laptops walioshinda zitakuza mbinu zao za ufundishaji.

Promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers iliweza kufikia shule za msingi 40 jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi walipata fursa adimu ya kujishindia baiskeli za kisasa pamoja na mabegi ya shule huku shule zao zikishinda Kompyuta pamoja na kompyuta mpakato (Laptop).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents