Michezo

PSG wazungumza na Zidane, United kumvuta Pochettino 

Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Zinedine Zidane wakijiweka sawa na uwezekano wa kocha wao Mauricio Pochettino kuondoka na kujiunga na Manchester United. (Le Parisien, via Metro)

Manchester City itapaswa kuongeza juhudi kumpa mkataba wa muda mrefu winga wa England Raheem Sterling, 26 ambaye anahusishwa na Barcelona, ili aweze kusalia klabuni hapo. (Telegraph – subscription required)

Manchester United imeungana na vilabu vingine, vikiwemo Tottenham na Newcastle United, kutaka saini ya mshambuliaji Mserbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina. (Mail)

Ralf Rangnick anatarajiwa kuwa kocha wa muda wa Manchester United lakini awali alikataa ofa kutoka klabu hiyo ya Old Trafford kabla ya kukubali masharti mapya ya mkataba huo. (Manchester Evening News)

Manchester United bado inamsaka Pochettino kuchukua mikoba ya umeneja msimu unaokuja, licha ya kuwasili kwa Rangnick. (90 Min)

Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26, anawaniwa na Manchester United kama mbadala wa Paul Pogba, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford unakwenda kumaliza mwishoni mwa msimu. (Fichajes – in Spanish)

Barcelona wanafikiria kutupa ndoano kumsajili mshambuliaji wa Basel Arthur Cabral lakini itabidi wauze baadhi ya wachezaji kabla ya kuu kupeleka ofa kwa mbrazil huyo mwenye miaka 23. (Goal)

Mkataba wa winga wa Croatia Ivan Perisic pale Inter Milan unakwisha June 2022 na nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 anasema “chochote kinawezekana, ngoja tuone wiki chache zijazo” alipoulizwa kuhusu mustakabali wake. (Mediaset Infinity, via Football Italia)

Inter Milan wanamatumaini kwamba kiungo wake Mcroatia Marcelo Brozovic,29 atasaini mkataba mpya, mkataba wske wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (90 Min)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents