HabariSiasa

Punguzo la bei ya Unga Kenya ni siasa kuelekea uchaguzi au uamuzi wa Serikali??

Tangazo la wizara ya Kilimo nchini Kenya kwamba bei ya unga wa mahindi itapunguzwa kwa wiki nne kutoka shilingi 230 hadi shilingi 100 siku 20 kabla ya uchaguzi mkuu limezua maswali mengi kuhusu afueni .

Wengi hasa mitandaoni wamehoji nia ya serikali wakati huu ikizingatiwa kwamba wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia bei ya juu ya unga kwa wiki kadhaa sasa bila kupata matumaini ya msaada wowote kutoka kwa upande wa serikali .

Punguzo hilo ambalo ni la takriban asilimia 60 litadumu kwa wiki nne tun a huenda bei ikarejea kuwa ile ya juu baada ya mpango huo wa ruzuku kati ya wizara ya kilimo na wasagaji nafaka kuisha.Mpango wenyewe haujawekwa wazi na duru zinaarifu haujakamilishwa lakini utafanikishwa . Tathmini katika sehemu nyingi za kuuza bidhaa huo inaonyesha bei haijapunguzwa ..

Mpango huo wa ruzuku ya mahindi hasa wakati huu wa kampeni umechukuliwa na baadhi kama hatua ya Rais Kenyatta, ambaye anamuunga mkono Raila Odinga wa Azimio la Umoja-kuwashawishi wa piga kura wakati huu ambapo wengi wamekuwa wakilalamikia gharama ya juu ya maisha.

Serikali pia imeondoa tozo zote zinazotozwa kwa mahindi kutoka nje ya nchi.

Wasagaji watawauzia wauzaji begi ya pakiti 12 za unga wa mahindi wa kilo 2 kwa Sh1,080, ambayo ina maana ya Shilingi 90 kwa pakiti.Serikali nayo itawafidia Sh1,120 kwa pakiti 12 za unga, au Sh93 kwa moja.

th

Naibu Rais William Ruto amemshutumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kucheza siasa na unga wa mahindi baada ya serikali kuchukua hatua zitakazopunguza bei ya bidhaa hiyo .

Akihutubia mikutano ya kando ya barabara jijini Nairobi, ambayo ina wapiga kura milioni 2.4, Dkt Ruto alisema Mkuu wa Nchi aliingilia tu kuchukua hatua hiyo kama chombo cha kampeni kwa sababu uchaguzi umekaribia.

“Hii ni serikali ile ile ambayo hapo awali ililaumu bei ya juu juu ya bidhaa kwa vita vya Ukraine na Urusi. Vita bado vinaendelea, kwa nini uliwaacha Wakenya wateseke kwa muda mrefu hivyo?” Ruto alihoji

“Nimesikia wakisema watapunguza gharama ya unga. Mwenyekiti wa Azimio (One Kenya Coalition) ndiye Rais na Raila (Odinga) ndiye anayepeperusha bendera. Ni tofauti gani unaweza kutarajia kutoka kwake? Serikali inataka kupunguza bei ya unga kwa sababu uchaguzi umekaribia,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents