Habari

Putin atalipa – Biden kuhusu Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa anafikiria mwenzake wa Urusu Vladimir Putin “ataivamia” Ukraine, lakini hataki “vita kamili”.

Joe biden

Alipoulizwa kuhusu tishio la uvamizi wa Urusi, katika mkutano na waandishi habari alisema: “Nadhani ataingia, lazima afanye kitu.”

Lakini alionya kwamba kiongozi huyo wa Urusi atalipa “gharama kubwa” kwa “kuchokoza” Magharibi.

Moscow inapinga madai ya kupana kushambulia au uvamizi lakini imeongeza vikosi vyake.

Inakadiriwa kuwa karibu wanajeshi 100,000 wamepiga kambi karibu na mipaka ya Ukraine.

Maafisa wa Ikulu ya White House baadaye walitoa taarifa kufafanua msimamo wa Marekani, baada ya baadhi ya waandishi wa habari katika mkutano huo kumhoji Bw Biden kuhusu iwapo Marekani ingeruhusu uvamizi mdogo wa Ukraine kufuatia maoni yake.

Ukraine tension: Blinken says Russia could attack at short notice - BBC News

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano usiku, katibu wa habari wa Ikulu ya White House, Jen Psaki alisema: “Iwapo jeshi lolote la Urusi litavuka mpaka wa Ukraine, huo ni uvamizi mpya, na hatua hiyo itakabiliwa haraka na Marekani, Nchi na Washirika wetu.”

Urusi imetoa masharti kadhaa kwa serikali za Magharibi, ikiwa ni pamoja na kwamba Ukraine haipaswi kamwe kujiunga na Nato na kwamba shughuli za kijeshi za muungano huo wa kujihami zinapaswa kuwa ndogo katika nchi wanachama ikiwa ni pamoja na Poland.

Mazungumzo kati ya nchi za Magharibi na Urusi wiki jana yalishindwa kufikia mwafaka, huku baadhi ya matakwa ya Moscow yakikataliwa kwa madai kwamba hayana msingi.

Urusi ilichukuwa rasi ya Crimea ya Ukraine mwaka 2014 baada ya kupinduliwa kwa serikali inayoiunga mkono Urusi nchini Ukraine.

Imewaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi wanaodhibiti sehemu za mashariki mwa Ukraine katika vita vikali vya umwagaji damu na vikosi vya serikali.

Kuna hofu kuwa mzozo huo , ambao ulisababisha vifo vya watu karibu 13,000 na kusababisha karibu watu milioni mbili kutoroka makwao, huenda ukatibuka tena, kutokana na jeshi la Urusi kuingilia kati kwa uwazi..

Putin ‘atajaribu nchi za Magharibi’

Alipoulizwa maoni yake kuhusu nia ya Bw Putin, Bw Biden alisema: “Je, nadhani atajaribu nchi za Magharibi? Ajaribu Marekani na Nato kwa kiasi kikubwa awezavyo? Ndiyo, nadhani atafanya hivyo lakini nadhani atalipa gharama kubwa.”

“Hajawahi kuona vikwazo kama vile nilivyoahidi vitawekwa iwapo atavamia Ukraine,” Bw Biden alisema, akiongeza kuwa kiwango kamili cha adhabu kitategemea ukubwa wa uvamizi wowote.

Alipoulizwa jinsi alivyokuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa mzozo wa Ukraine kusamba hadi katika mataifa jirani ya wanachama wa Nato, alisema: “Vita pekee ambayo ni mbaya zaidi kuliko ile iliyokusudiwa ni wakati ambapo haijakusudiwa na ninachojali ni kwamba hili linaweza kwenda vibaya.

“Natumai Vladimir Putin anaelewa kwamba, anaelekea kutibua vita vkamili vya nyuklia, na hayupo katika nafasi nzuri sana ya kuitawala dunia. Na kwa hivyo sidhani kama anafikiria hivyo, lakini kuna wasiwasi.”

Pia alisema kuwa ni “muhimu sana” kwa washirika wa Nato kuwa pamoja wakati huu ambako kuna tishio la shambulizi la Urusi.

Bw. Biden amesema kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Urusi na kwamba mkutano kati yake na Bw. Putin bado “unawezekana.”

Waziri wa Mambo Nje wa Marekani US Antony Blinken anatarajiwa kukutana na Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Urusi wa Sergei Lavrov mjini Geneva siku ya Ijumaa,baada ya kuzuru Ukraine nakufanya mazungumzo na washirika wa Ulaya mjini Berlin.

Akizugumza mjini Kyiv,Bwa Blinken alisema Urusi inaweza kushambulia Ukraine “ghafla” na kuonya tena juu ya vikwazo vikali ikiwa hilo litafanyika.

Biden afichua mvutano wa umoja wa Nato

Maafisa wa utawala na washirika wa Nato hawawezi kufurahishwa na Biden kuelezea tofauti za Nato hadharani bila kusita. Taswira iliyojengwa kwa umma imekuwa juu ya umoja.

Lakini rais amefichua nyufa zilizopo, na kuibua swali ikiwa anampa Putin ruhusa ya uvamizi.

Sasa rais ameeleza wazi kile ambacho kila mtu alijua faraghani – kwamba Nato imeungana kuamua hatuaitakayochua dhidi ya uvamizi, lakini sio uvamizi: “Kuna tofauti katika kile ambacho nchi ziko tayari kufanya kulingana na kile kinachotokea

“Ikiwa majeshi ya Urusi yatavuka mpaka na kuwaua Waukraine, hiyo inabadilisha kila kitu. Inategemea atafanya nini kupata umoja wa Nato.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents