Rado amchana Nay wa Mitego,Diamond na Steve Nyerere wapewe maua yao(Video)
Akifanya mahojiano na @el_mando_tz msanii huyo wa Bongo Movie @radomanking amedai Rapa wa Bongo Fleva @naytrueboytz kukosoa Serikali inaonyesha namna gani ana uwezo mdogo wa kufikiria.
Anaongeza kuwa anasema yale mabaya tu kwani hakuna mazuri aliyoyafanya Rais Samia?? Mbona yale hayasemi??
msanii huyo wa Bongo Movie @radomanking amejibu kuhusu wasanii wengi kuwa machawa na kushindwa kuwasema Wananchi.
@radomanking amezungumza mengi sana ambayo wasanii wanayafanya ili watu hawataki kuyazungumza kwenye Jamii.
Lakini pia yeye na @jimmymafufu mwaka 2020 walikuwa Chadema na waliahidiwa kuteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya lakini baadae wakaona hamna kitu wakarudi CCM.
Mahojiano yote ya @el_mando_tz na @radomanking yapo kwenye ukurasa wetu wa YouTube wa Bongofive.