Mahojiano

Rado “Hakuna msanii Tanzania anaweza kuigiza kama mimi, Ndio msanii pekee niliyecheza aina zote za Uigizaji” – Video

Rado "Hakuna msanii Tanzania anaweza kuigiza kama mimi, Ndio msanii pekee niliyecheza aina zote za Uigizaji" - Video

Msanii wa Bongo Movie RADO ameeleza sababu za kupotea kwake kwenye tasnia ya Bongo Movie na kufunguka kila kitu
Mbali na hilo RADO ameongeza kuwa licha ya kuonekana yupo kimya sana lakini anajiamini sana na kile anachofanya na HAKUNA MSANII ANAYEWEZA KUINGIZA KAMA YEYE.


RADO ameongeza kuwa “Hata nikifa leo hakuna msanii ananifikia hata robo mana mimi nimecheza katika mionekano tofauti kushinda msanii yeyote Tanzania “

Bwana Rado pia ameongelea suala la Wasanii kuonekana kupelekeshwa na msanii mmoja ambaye anashindwa hata kuwatetea wenzake Kwa Viongozi zaidi ya kuishia kupiga picha tu”

Lakini Pia katika suala la wasanii wa Bongo movie kuonekana wanapenda kulalamika Rado amekubali na kusema ni kweli kwa sababu mara nyingi mtu ambaye huaminiwa na wenzake ili awe mtetezi wao au kiongozi wao anashindwa kuwatetea na kubaki wao kuonekana kulalamika kumbe hakuna mahali pa kutoa hisia zao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents