FahamuHabariSiasa

Raia wa Kitanzania wawili hawajulikani walipo Israel, wengine kurudishwa nchini

Tanzania inapanga kuwarudisha nyumbani raia wake wote wanaoishi Israel na mataifa jirani.

Taarifa iliyotolewa na idara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini humo inasema uamuzi huo umewadia baada ya wao kutathmini hali ya usalama nchini Israel.

“Tunawashauri wale walio tayari kurejea nyumbani kujiandikisha kupitia ubalozi wa Tanzania ulioko Tel Aviv kabla ya mwisho wa Oktoba 15,” ilisema taarifa hiyo.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania mjini Tel Aviv umeiambia BBC kuwa hadi jana bado wanatafuta taarifa kuhusu raia wawili waliotoweka baada ya mashambulizi ya mwishoni mwa juma lililopita na wanamgambo wa Hamas kusini mwa Israel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents