HabariSiasa

Raila Odinga aonywa, maandamano yako mwisho jumatatu

­Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua alimuonya Raila Odinga dhidi ya kufanya maandamano mfululizo nchini Kenya, akisema Jumatatu, Aprili 3 itakuwa siku ya mwisho ya maandamano kabla ya serikali “kuthibitisha mamlaka yake”, gazeti la The Standard limeandika.

Bw.Gachagua alikuwa akizungumza huko Malava, Kaunti ya Kakamega wakati wa hafla ya kumshukuru Mbunge wa eneo hilo Injendi Malulu.

“Ninataka kuwahakikishia watu wa Kenya leo kutoka Kaunti ya Kakamega kwamba kesho hakuna mtu, na narudia hakuna mtu, atakayeruhusiwa kuharibu mali popote katika Jamhuri ya Kenya,” Gachagua alisema katika hotuba yake.

Aliendelea kunukuliwa; “Ninataka kuwatahadharisha vijana ambao wamekuwa wakijinufaisha na ghasia zilizoibuliwa na Raila kuiba mali, kuwapiga watu na kupora mali, kwamba Jumatatu, Aprili 3 ndiyo siku yao ya mwisho kufanya hivyo.

“Sheria za nchi hii ziko wazi. Anachoongoza Odinga si maandamano tena. Ni vurugu za baada ya uchaguzi, wizi, wizi, wizi na unyang’anyi kwa kutumia vurugu. Hao ni wahalifu.

“Ikiwa wanajali, kuangalia kanuni za sheria, wangejua athari yake ni kubwa sana. Jumatatu, Serikali ya Jamhuri ya Kenya itasisitiza mamlaka yake katika kulinda maisha na mali na kuzingatia utawala wa sheria. Ninatoa tahadhari hiyo kwa vijana hao kwamba haitakuwa biashara kama kawaida. Hali hiyo haiwezi kutokea tena, Ni makosa, ni kinyume cha maadili na haikubaliki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents