Habari

Rais aliyepinduliwa nchini Mali aaga dunia

Rais wa Mali aliyeondolea madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76 , familia yake na rafiki zake wamesema.

Tsohon Shugaban Mali Boubacar Keita ya rasu | Labarai | DW | 16.01.2022

Miaka miwili iliopita aliugua kiharusilakini chanzo cha kifo chake siku ya Jumapili hakikuweka wazi.

Alifariki mwendo wa saa tatu saa za Uingereza nyumbani kwake mjini Bamako , mmoja wa ndugu yake aliambia chombo cha Habari cha AFP.

Bwana Keitaaliiongoza Mali kwa miaka saba hadi 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.

Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake.

Bwana Keitaalihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu kutoka 1994 hadi 2000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents