Siasa

Rais Kenyatta kuwa rais wa kwanza Afrika kukutana na rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kufanya mkutano wake wa kwanza wa ana kwa ana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kesho Alhamisi wakati ambapo vita na mzozo wa kibinadamu vikifukuta nchi jirani ya Ethiopia.

Mazungumzo hayo katika ikulu ya White House yanafanyika wiki kadhaa baada ya Biden kusaini amri ya rais ambamo anaitishia vikwazo dhidi ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na viongozi wengine wanaojihusisha na mzozo wa Tigray, iwapo hawatachukua hatua za kuumaliza mzozo huo wa miezi 11.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atakutana na rais wa Marekani Joe Biden wakati akimaliza ziara yake ya siku mbili nchini Marekani. Rais Kenyatta atakuwa rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana na rais Biden tangu kiongozi huyo aapishwe mwaka huu.

Msemaji wa Ikulu ya Kenya amesema viongozi hao wawili watajadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya amani , usalama na mabadiliko ya tabia nchi.

Jumanne, Rais Kenyatta aliwaongoza viongozi wa biashara kusaini mikataba kadhaa ya uwekezaji wa biashara ndogo na wastani pamoja na miradi ya usafirishaji na nishati safi.

Marekani inaiona Kenya kuwa mshirika sahihi katika kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki mwa Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents