Rais, Makamu kutoa vibali vya kutoka nje ya mkoa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amewapiga marufuku wakuu wa mikoa na Wakurugenzi kutoka nje ya mkoa bila kibali cha Rais, Makamu au Waziri Mkuu.


Ummy amesema hayo leo Jumanne Oktoba 12, 2021 wakati akifafanua namna Wizara yake itakavyotumia mkopo wa IMF kutekeleza miradi mbalimbali na kwamba Viongozi wa Mikoa na Wakurugenzi wanatakiwa kuepuka safari zisizo za lazima za kutoka nje ya mkoa isipokuwa kwa kibali ili kufanikisha usimamizi wa miradi hiyo.

Lakini kwa sababu tunajambo hili kubwa, ninawaelekeza viongozi wote wa Serikali ndani ya Tamisemi, ngazi ya mikoa, wilaya na halmashauri kuepuka safari zisizo za lazima zinazohusu kutoka nje ya mkoa wako isipokuwa kwa kibali cha viongozi wakuu wa nchi. Mkuu wa mkoa ukitaka kutoka ndani ya mkoa wako kipindi hiki lazima upate kibali cha Rais, kibali cha Makamu wa Rais au Waziri Mkuu,” Waziri Ummy.

Katika kutilia msisitizo agizo hilo Waziri Ummy amesema hata yeye akitaka kukutana na viongozi hao wa mikoa itabidi aombe kibali kwa viongozi wake ambao ni wakuu wa nchi.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button