Rais Mstaafu Kikwete Kisarawe kwa DC Jokate, acheza basketball na wanafunzi (Video)

Rais Mstaafu Mhe @jakayakikwete Jumanne hii alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ujenzi wa kiwanja cha basketball ambacho kinajenga katika shule ya Minaki Wilayani Kisarawe kwa juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe @jokatemwegelo ambaye aliwatafuta mdau Giants Of Africa, Masai Ujiri GM wa timu inayochezea ligi ya NBA Toronto Raptors.


Kikwete ambaye ni mpenzi wa mpira wa kikapu na yeye siku ya leo aligeuka mwalimu kwa wanafunzi ambao walicheza mechi kwaajili ya kuonyesha uwezo wao, ambapo katika hotuba yake aliwataka wadau wa michezo hiyo kuwekeza kwa walimu pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wa michezo.
https://youtu.be/SCI5PTvQsew

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button