Rais Mstaafu Kikwete: Mkapa alichukia umasikini, alitaka ifikapo 2025 kipato cha Mtazania kiwe dola 3000 (Video)

Rais Mstaafu Kikwete akiwa katika mazishi ya Rais Mstaafu Hayati Mkapa, amesema hayati alikuwa anaumizwa sana na umasikini.

“Mkapa alitengeneza dira ya 2025, kwamba ifikapo 2025 Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati, na pato la wastani la kila Mtanzania liwe dola 3000 ndio tamaa yake”

“Tumeshafika kwenye uchumi wa kati lakini hatujafika kwenye lile ambalo mzee Mkapa alilikusudia la dola 3000 kwa wastani wa kila Mtazania ufikapo mwaka 2025. Mimi naamini tukimpa nafasi tena Magufuli na anaamini atapata tutafika kule”

“Bado ni safari ndefu tupo kwenye 1080 sasa, kwenye dola 3000 bado tunadaiwa kwenye 1920”

Related Articles

Back to top button