HabariUncategorized

Rais Mugabe amchimba mkwara Trump ‘Hakuna taifa dogo kijeshi’

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemuonya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa asijidanye kwa ulimwengu huu wa teknolojia kwamba Marekani itakuwa ndio nchi yenye nguvu pekee duniani ya kutengeneza silaha nzito za kivita.

Robert Mugabe

Mugabe ameongea hayo Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kurejea nchini Zimbabwe akitokea Marekani kwenye mkutano wa umoja wa Mataifa ambako Rais Trump alitamka kuwa endapo atapata ruhusa ya kuishambulia Korea Kaskazini basi ataiangamiza kwa muda mfupi.

Mugabe amesema kwa sasa kila nchi inauwezo wa kumiliki silaha za nyuklia na sio kwa nchi kubwa hiyo dhana imekufa huku akihimiza kila taifa lijitegemee kiutawala pasi kuingiliana.

Hakuna nchi inayoruhusiwa kuipelekesha nchi nyingine kwenye masuala ya kijeshi nadhani kila nchi ijitegemee, kila nchi ina nguvu yake hakuna taifa dogo kijeshi, kwa hiyo ningependa kumuonya (Trump) awe makini,“amesema Rais Mugabe kwenye mahojiano yake na gazeti la kiserikali la  Herald newspaper wakati akihutubia wanachama wa Chama tawala cha Zanu-PF waliojitokeza kumpokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents