HabariSiasa

Rais Museveni amesema mtoto wake hatajihusisha na Twitter

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema mtoto wake, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, hataweza tena kutoa maoni kuhusu masuala ya serikali kwenye mtandao wa Twitter.

Hatua hii inafuatia baada ya mtoto wake huyo kuibua dhoruba katika mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita.

Jenerali Kainerugaba mwenye umri wa miaka 48, aliandika kwenye Twitter kuhusu kuvamia nchi jirani ya Kenya na kuuteka mji mkuu wa Nairobi, katika muda wa wiki mbili.

Rais Museveni baadaye aliwaomba radhi Wakenya kutokana na ujumbe huo wa twitter. “Atajiondoa kwenye Twitter. Tunalijadili hili. Twitter sio tatizo. Tatizo ni kile unachoandika kwenye Twitter,” Rais Museveni alikiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda siku ya Jumatatu.

Aidha aliongeza: “Kuzungumza kuhusu nchi nyingine na siasa za upendeleo za Uganda ni jambo ambalo hapaswi kufanya na hatalifanya.” Kiongozi huyo mkongwe alisema mtoto wake alikuwa huru kuandika kwenye twitter ujumbe wowote kuhusu “michezo au mada ambazo hazina utata”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents