Siasa

Rais Ramaphosa: Hizi ghasia na vurugu ni za kupangwa (+ Video)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ghasia na vurugu zilizotokea nchini humo zilikuwa ni za kupangwa. Amesema hayo akiwa huko Kwazulu Natal wakati akikagua uharibifu uliosababishwa na maandamano mabaya zaidi kutokea katika historia ya demokrasia ya nchi hiyo.

Rais Ramaphosa amekiri pia kwamba wasimamizi na watekelezaji wa sheria wangefanya vizuri zaidi katika kudhibiti ghasia hizo. Rais Ramaphosa, amekiri kwamba hatua zilizochukukuliwa awali zilipoaswa kuangaliwa upya.

Mamia ya maduka katika majimbo mawili ya nchi hiyo yalivamiwa na miondo mbinu iliharibiwa vibaya katika ghasia mbaya zaidi kutokea katika utawala wake. Rais huyo alisema uporaji uliofanywa ulipangwa na watu ambao hawana nia njema na demokrasia ya Afrika Kusini, ingawa hajafafanua kwa undani zaizi kauli yake hiyo.

Watu 117 wamethibitishwa kufariki dunia katika kipindi cha wiki moja cha ghasia hizo wakati maelfu ya watu wakivamia maduka na kufanya uharibifu mkubwa wa miundo mbinu.

Maandamano hayo yalianza wakati rais wa zamani wa taifa hilo Jacob Zuma alipojisalimisha na kuwekwa jela kwa kudharau Mahakama kwenye kesi yake ya msingi ya rushwa, lakini maandamano hayo yalienda mbali zaidi na kushindwa kudhibitika na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola za kimarekani.

Bofya hapa kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CRZEy1SDFz0/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents