HabariSiasa

Rais Ruto aagiza mhubiri aliyeamuru watu wafunge hadi kufa ashitakiwe

Rais wa Kenya William Ruto ametaka kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie ambaye aliwataka wafuasi wake kufunga hadi kufa

Rais amemtaja mhubiri huyo kuwa gaidi. Matamshi yake yanakuja muda mfupi baada ya Polisi kupata mwili mmoja zaidi kutoka kwenye kaburi la pamoja karibu na mji wa pwani wa Malindi. Hii inafikisha 40, idadi ya waliofukuliwa, na idadi ya vifo ikifika 48.

Polisi wameviambia vyombo vya habari kwamba miili miwili zaidi imeonekana na itafukuliwa katika muda mfupi ujao.

Maafisa wakuu wa usalama wakiongozwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome na Mkuu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin wanatarajiwa kujiunga na timu ya wachunguzi katika eneo Shahola palipopatikana makaburi ya kina kifupi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents