Habari

Rais Samia aagiza katika tamasha la kitaifa la utamaduni mwezi Mei kuwe na ushirikishwaji wa machifu na viongozi wa kimila

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa katika tamasha la kitaifa la utamaduni litakalo kutanisha mikoa yote mwezi Mei, kuwe na ushirikishi mzuri wa machifu na viongozi wa kimila.

Katika tamasha kubwa la kitaifa la utamaduni litakalo kutanisha mikoa yote mwezi Mei, naagiza kuwe na ushirikishi mzuri wa machifu na viongozi wa kimila. Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na watu wengine mashuhuri waalikwe ili waje kuona utamaduni wetu- Rais Samia Suluhu Hassan

Utamaduni ni utambulisho wa taifa, utamaduni ni ajira, utamaduni ni kivutio cha utalii na ni uchumi. Nchi inaheshimika kutokana na utamaduni wake. Tutangaze tamaduni zetu nzuri ili dunia izijue na ije kuziona – Rais Samia Suluhu Hassan

Tuendelee kukuza na kuendeleza vikundi vyetu vya burudani za kiutamaduni na kuzalisha kazi za mikono za utamaduni wetu – Rais Samia Suluhu Hassan

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents