Habari

Rais Samia achangia milioni 70 kwa Doris Mollel foundation

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amechangia Tsh. Milioni 70 kwa Doris Mollel Foundation, ambapo Tsh. Milioni 20 ameitoa kuwasaidia watoto njiti kupitia Doris Mollel Foundation na pia amenunua vifa tiba vya kuwasaidia Watoto Njiti vyenye thamani ya Tsh. Milioni 50.

Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ambaye yeye pia alizaliwa Mtoto njiti, Doris Mollel amemshukuru Rais kwa msaada huo ambapo amesema ameutoa siku mwafaka kwakuwa leo ni Siku ya Mtoto Duniani na Doris Mollel Foundation inaitumia siku hii kutoa misaada mbalimbali ..

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dr.Godwin Mollel amesema fedha hizo ni za Rais mwenyewe kutoka kwenye mshahara wake na amemshukuru kwa kuchangia lakini amesema Serikali kwa ujumla kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuwasaidia Watoto njiti na Wanawake wanaojifungua Watoto njiti.

Doris Mollel Foundation leo imeadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo kwa kawaida huadhimishwa mnamo tarehe 17 Novemba kila mwaka, kwao maadhimisho hayo yamefikia kilele leo November 20, 2022 ambayo ni Siku ya Mtoto Duniani na yanafanyika katika viwanja vya Robanda, vilivyopo katika Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents