Habari

Rais Samia aelekeza wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo kulipwa fidia bila usumbufu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza wananchi wote wanaopisha miradi ya maendeleo kulipwa fidia zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.

Silaa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ulipaji fidia za wananchi katika kupisha Mradi wa Uchimbaji wa Madini ya Nickel unaofanywa na Kampuni ya Tembo Nickel katika Halmashauri ya Manispaa ya Ngara mkoani Kagera.

Katika ziara hiyo ambayo imehudhuriwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

Aidha Silaa ameitaka Kampuni Tembo Nickel kulipa fidia za wananchi kwa haraka kabla ya tarehe 25 Desemba 2023.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents