Habari

Rais Samia aguswa na Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi

Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.

Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

Amina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents