Rais Samia aijubu sauti ya Khaan wa Clouds

Kufuatia story ambayo aliifanya Mtangazaji wa #cloudsmedia @Khaan_Mbarouk kupitia ukurasa wake wa #instagram kuhusu hali mbaya ya Msikiti ambao unatumiwa katika sala na Ibada na waumini ambao ni wakazi wa kijiji cha Milo, kata ya Vigwaza kitongoji cha Migude Mkoani Pwani, Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. @samia_suluhu_hassan ameguswa na kumtaka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Waleed Alhad Pongwa kufika katika eneo la msikiti huo na kutazama mahitaji muhimu ili ukarabati wa msikiti huo uweze kuanza mara moja.
Mapema mchana wa leo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Waleed Alhad Pongwa amefika eneo la msikiti huo kutekeleza agizo la Rais, ameketi na viongozi wa Msikiti na Serikali ya Kijiji kujua changamoto na mahitaji muhimu ili ukarabati uweze kuanza mara moja.
Sheikh Waleed amewataka wanahabari wengine kuiga mfano wa @Khaan_Mbarouk katika kufanya mambo yanayoigusa jamii na kuleta utatuzi keenye changamoto mbalimbali kama ambavyo amekuwa akifanya