HabariSiasa

Rais Samia amteua Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa mrithi wa Mabeyo

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amefanya uteuzi wa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania akichukua nafasi ya Mkuu aliyemaliza muda wake CDF Venance Mabeyo.

Rais amemteua Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuchukua nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Jeshi.

Mbali na hilo Rais amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents