Bongo5 ExclusivesHabariSiasa

Rais Samia amuapisha Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda na kuzungumza haya

Jenerali Jacob John Mkunda leo Juni 30, 2022 ameapa rasmi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.  @SuluhuSamia katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Wakati wa uapisho huo Rais amesema kuwa: ““Nikushukuru sana Jenerali Mabeyo kwa kazi nzuri uliyoifanya katika utumishi wako, nilipokuwa nazungumza nawe jana ulisema ni miaka 40 na kidogo umetumikia katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Hongera sana”

“Jenerali Mabeyo umefanya kazi yako kwa uadilifu mkubwa, umetumikia cheo chako kwa jitihada kubwa na leo unamaliza na kukabidhi kwa wengine. Tunakushukuru sana na kukupongeza sana”

“Jenerali Mabeyo unamaliza utumishi ukiwa kijana na ukiwa na nguvu, na kwa maana hiyo tutaendelea kukuteua. Tutaendelea kukupa majukumu ili uendelea kutusaidia. Nadhani jioni ya leo kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi tutakusikia kwenye bomba, Tunakushukuru sana, tunakupongeza sana na kukuomba sana Jenerali Mabeyo uendelee kulitumikia Taifa lako” – Rais Samia Suluhu

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents