Habari
Rais Samia apeperusha bendera kuashiria kuruhusu magari kupita daraja la J.P Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan akipepea pendera kuashiria kuruhusu Magari kuanza kupita katika Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa Km 3 na Barabara Unganishi za urefu wa Km 1.66.
Rais Samia ameyafanya hayo leo Juni 19, 2025 wakati akizindua rasmi daraja hilo ambalo linaunganisha Tanzania na nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.
Wakati wa uzinduzi huo mamia ya watu wamejitokeza na kuonesha kifurahishwa na tukio hilo ambalo litachochoea ukuaji wa uchumi katika Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.
Written by Janeth Jovin