Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki na kuhutubia katika Mkutano wa Ngazi ya Juu unaohusu Ukuaji wa Viwanda na Kilimo cha Kisasa Afrika kwenye Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Rais Samia ameshiriki katika mkutabo huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha China mjini Beijing, tarehe 5 Septemba, 2024.