Rais Samia ataka Kilimanjaro kudumisha amani, ili serikali ifikiri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoani Kilimanjaro kudumisha amani ili kuipa serikali nafasi ya kutatua changamoto zao.

Rais Samia ameyasema hayo leo baada ya uzinduzi wa barabara ya lami ya Sanya Juu – Elerai, Siha Mkoani Kilimanjaro yenye refu wa kilometa 32.2

Akihutubia, Rais amewaambia wananchi wa Siha endapo wakidumisha Amani na Upendo, serikali itapata wasaa mzuri wakufikiri wapi p akupata fedha ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.

Mbali na hayo Rais Samia amewataka viongozi kusimamia utatuzi wa changamoto zinazotatuliwa na Serikali Kuu pamoja na Chama kusudi zisijirudie mara kwa mara.

Akiwekea msisitizo kauli yake, Rais Samia amesema haipendezi kukuta changamoto za wananchi zinajirudia kila wakati hata baada ya kutatuliwa na Serikali Kuu, na kuongeza kwamba ni vyema serikali ya eneo husika ikashirikiana na mkoa katika kumaliza changamoto hizo.

Rais Sami apia anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Mto Rau-Manispaa ya Moshi ambalo ujenzi wake utagharimu Millioni 910.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button