Habari

Rais Samia ataka taarifa ya kina haraka za waliomuua mzee Kibao wa Chadema

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amegiza Vyombo vya Uchunguzi kumpatia taarifa ya kina haraka kuhusu tukio baya la mauaji ya Kiongozi wa Chama cha DEmokrasia na Maendeleo (CHADEMA),  Ali Kibao na mengine ya namna hiyo.

Rais Samia amesema “Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi, Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii”

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao, natoa pole kwa Viongozi wa Chama hicho, Familia ya Mzee Kibao, Ndugu, Jamaa na Marafiki.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents