HabariSiasa

Rais Samia atangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi ya kila mwaka

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) Mkoani Morogoro ambapo amewaambia Wafanyakazi kuwa kuanzia mwaka huu zile nyongeza za mishahara za kila mwaka ambazo zilisitishwa kwa muda mrefu, zinarudi tena.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Mwaka huu mbali na upandishaji wa posho, tumejiandaa pia kupandisha madaraja kutaendelea, vyeo vitaendelea kupandishwa, madaraja ya mserereko ambao hakuwapata mwaka uliopita mserereko upo mwaka huu”

“Kuna nyongeza za mishahara za mwaka ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zimesitishwa nikaona mwaka huu tuzirudishe, kwahiyo Wafanyakazi wote mwaka huu kuna nyongeza za mishahara za kila mwaka na tunaanza mwaka huu na zitaendelea kila mwaka”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents